Katika kujenga afya ya mtoto mdogo ni muhimu mama au mlezi kuwa na elimu ya kutosha kujenga msingi mzuri wa afya ya mtoto kwani afya bora inaanza kujengwa akiwa na umri kuanzia miezi sita na kuendelea anapoanza kupewa chakula cha ziada.

Kipindi cha miezi sita ya mwanzo kasi ya ukuaji ya maendeleo ya mtoto huwa ni kubwa hivyo kuna mambo kadhaa tunatakiwa kuzingatia kujenga afya ya mtoto mwenye afya bora.

Katika kipengele hiki ntazungumzia baadhi ya mambo yote ya msingi ya kuzingatia katika kujenga afya bora ya mtoto kuanzia umri wa miezi sita na kuendelea kwa kuzingatia zaidi virutubisho.

Lishe bora yenye mlo kamili kwa mtoto ni muhimu sana katika kujenga afya kwani inafanya miili yetu kuwa na nguvu, kuboreshwa, kufanya mwili kufanya kazi vizuri katika mifumo yote ya mwili na kutulinda na magonjwa.

Mlo kamili wenye virutubisho vyote muhimu kama protini, wanga, vitamini, madini, fiber, maji na mafuta unachochea ukuaji mzuri wa maendeleo ya afya nzuri ya mtoto kwa ujumla.

Mchango wa familia katika malezi bora, wana familia wote wanaoishi na mtoto mdogo ni muhimu sana mchango wao katika kujenga afya ya mtoto, kwani watoto wanahitaji kutunzwa, kuoneshwa mapenzi, kufanyiwa hisani na kuelimishwa taratibu.

Wana familia ambao hawamjali mtoto wanamfokea, wanamtisha, wanampiga hovyo hovyo bila msingi wowote au kumfanyia vitendo vya ukatili huchangia sana kudhorotesha afya ya mtoto na maendeleo yake ya ukuaji kimwili na kisaikolojia.

Mazingira mazuri ya mtoto kucheza, mtoto kushiriki katika michezo na wenzake kuna mjenga kimwili na kiakiri anaimarisha mifupa na misuli yake kwa kucheza na hivyo kiafya inamjenga vizuri kimwili na kisaikolojia.

Mtoto anayefungiwa ndani ya nyumba yenye geti peke yake bila watoto wakucheza nao na hakuna mazingira mazuri ya kucheza na wenzake kisaikolojia hawezi kuwa sawa na kimwili hawezi kuwa na afya. 

Inapendekezwa kama hakuna mazingira mazuri ya mtoto kucheza na wenzake mara moja au mbili kwa wiki mpeleke mahali kuna watoto wenzake akacheze kuimarisha afya yake kimwili na kisaikolojia.

Usalama wa vyakula vya mtoto ni muhimu sana kuzingatia unapo nunua vyakula vya mtoto, maandalizi ya vyakula vya mtoto visiwe vimeharibika na kutengeneza sumu 'toxic' na wadudu 'pathogen' ambao anaweza kuwa virus au bakteria.

Vyakula vilivyoharibiwa na bakteria au wadudu vinaweza kupelekea kuharibu afya ya mtoto katika maendeleo yake ya ukuaji na kusababisha kutokuwa sawa kwa ubongo wake 'neurotoxicity' kutokana na kula vyakula vilivyoharibiwa na wadudu.

Hakikisha unanunua vyakula safi ambavyo havijaharibika na kuandaa vizuri katika hali ya usafi wakati wa kupika chakula cha mtoto.